Wednesday, March 4, 2009

Swahili Firefox: Be a part and Share the fun

Utajisikiaje kama nikikupa kompyuta ambayou haikulazimu kujua Kiingereza ili kuitumia. Sema iwe ya Kiswahili. Kompyuta yote ikawa ya Kiswahili. Najua, inaonekana kama haiwezekani.Inawezekana na ninao uthibitisho.


Kuswahilisha

Mwishoni mwa mwaka jana, timu ndogo ya watumiajo tabaruki wa Linux (tzLUG) walianza kazi kiswahilisha Firefox. Neno moja lipelekea mawili ambayo yalipelekea nyuzo ya matini na leo tumekamilisha 93% ya kazi yote. Sasa tunamalizi kilichobaki ili tutoe toleo la kwanza la majaribio tarehe 17 ya Machi.

Je wewe inaingia wapi? Unaweza jiunga kwenye uswahilishaji au ukafurahia kazi tulioifanya na kututumia maoni kwa vile tulivyoviruka ama marekebisho. Kwa sasa tunamalizi 7% ya marekebisho yaliyobakia ili iwe tayari kwa matumizi yako.

Tunatarajia kuwa na OpenOffice.Org (programu za ofisini kama Microsoft Office, ila ni imara zaidi ya MS Office na itakugharimu TZS 0/=) ifikiapo mwisho mwa 2009. Kwahiyo tungefurahia sana make tugepata jozi za mikono na macho toka kwako katika kukamilishsa zoezi hili. Kwa sasa bado hatujakamilisha mipango kwa ajili ya OpenOffice.Org. Programu moja baada ya nyingine na hivi karibuni tutakuwa na gawio kamili la Linux la Kiswahili.

Magawio ya Linux

Katika tzLUG, tunajitahidi kurahusisha upatikanaji wa magawio ya Linux. Kama unahitaji magawio ya Linux, tafadhali tifahamishe ili tupange jinsi ya kukupatia. Utaratibu wetu wa ugawaji si mzuri lakini tinaufanyia kazi.

Kwa sasa tunayo magawio yafuatayo:-

  * OpenSuse 11 - DVD
  * Fedora core 10 - DVD
  * CentOs linux - DVD
  * Ubuntu desktop 8.10 - CD
  * Ubuntu 8.10 server - CD
  * Ubuntu 8.04 - LTS - CD
  * Mythubuntu 8.10 - CD
  * Ubuntu studio 8.10 - CD

Tuna mpango wa kutuma mengine, kama kuna gawio unalitaka tufahamishe tufuta na kulituma. Kupata gawio wasiliana na Mratibu wa tzLUG kwa +255717566504 (Sebastian).

Magawio yafuatayo yatatumwa Ijumaa hii:-

  * Knoppix
  * Mandriva
  * Slackware
  * Linux Mint
  * FreeBSD - (sio Linux distribution but its Open Source)
  * 64 Studio - specialising in multimedia and digital content creation platforms

Juinge na tzLUG leo kupitia tzLUG Register na tugawane tukijuacho juu ya Linux, msaidie mtu ama pata msaada. Ni kwa ushirikiano ndio tutafanikisha. 

No comments:

Post a Comment