Baada ya kutafisri Firefox kwa miezi minne, niliamua kujikumbusha PHP kidogo. Kwa hiyo mwisho wa wiki huu likaipeka tovuti ya tzLUG shopping na kupiga pasi baadhi ya kurasa.
Kurasa nilizifanyia kazi zaidi ni ya kuonyesha Linux Distro tulizonazo na matoleo yake. Pia nimebadili muonekano wa tovuti nzima. Nimekurahisisha uchaguaji wa Linux na toleo unalolitaka. Sasa unaweza kupata FreeBSD na openSolaris, ambazo sio Linux ila ni chanzo huria (open source). Ushindwe wewe tu. Tafadhali kama una maoni usisite kunitumia. Pia nimeongeza ukurasa wa Review ambao utatumika kuonyesha kazi ambazo unaweza jaribu kabla ya toleo la mwisho.
Mwisho wa wiki ijayo, nitatengeneza kurasa ya miradi na kusakinisha Moodle ili tuweze kuwa na Online Course, tutaanza na Linux kwa Wabongo.
- Eclipse ikiwa na programu-jalizi la PHP, kama kihariri
- GIMP kwa ajili ya kuhariri na kutenegeneza picha na kodi za rangi
- Majaribio ya mefanyika kwe Swahili Firefox (RC1), Opera and Internet Explorer (ikiendeshwa juu ya VirtualBox OSE)
- gFTP imetumika kuhamisha mafaili kwenye seva
Ukiachana na Opera na Internet Explorer, programu zingine zote ni za chanzo huria (open source). Kama una maona maoni au maswali tafadhali usisite kuniuliza.
Kama Linux unayoitaka haipo basi tuambie na titaiweka